Kalenda ya Initial Coin Offering (ICO) husaidia wafanyabiashara na wawekezaji kufahamu mapema sarafu mpya zaidi za kidigitali zilizozinduliwa. Hili huwezesha wafanyabiashara na wawekezaji kuanza kuwekeza kabla bei hazijapanda, punde baada ya ICO kukamilishwa na uzinduzi kufanyika.
Kalenda ya ICO huonyesha ICOs zinazojiri, sarafu husika, na kundi la tasnia ambalo sarafu hizo zitakuwa. Pia, huonyesha urefu wa muda ambao ICO itachukua, pamoja na fedha zilizokusanywa.
Kuna miradi mipya ya sarafu za kidigitali inayoachiliwa mara kwa mara, na ingawa si miradi yote hufanikiwa, kalenda ya ICO huwapatia wafanyabiashara na wawekezaji taarifa mapema ya nini cha kutarajia. Pia huwapatia wazo la sarafu wanazoweza kufanyia utafiti ili kutambua kama mradi fulani utavutia kiasi kikubwa cha watu pindi utakapozinduliwa.
