Fahirisi za Hisa, zinazotolewa na TradingView, hutumia uwekezaji fulani wa kampuni wakilishi zinazoakisi hali ya soko la hisa kiujumla. Kuna aina tatu tofauti za fahirisi zinazoitwa fahirisi za kimataifa, kikanda na kitaifa. Fahirisi hujumuisha kati ya hisa kumi hadi mia moja, huku kila fahirisi ikihesabu ukubwa wa wastani tofauti.
Fahirisi hizi za hisa zinaweza kufanyiwa biashara kama vifaa vya fedha vinavyojitegemea. Fahirisi zilizoorodheshwa hapa ni fahirisi kubwa zinazowakilisha yafuatayo:
- S&P 500 – ‘Standard & Poors 500’ hujumuisha kampuni 500 kubwa zilizoorodhesha hisa zake katika Soko la Hisa la New York (NYSE) na ‘National Association of Securities Dealers Automated Quotations’ (NASDAQ) kulingana na mtaji wa soko.
- Dow 30 – ‘Dow Jones Industrial Average Index’ ni wastani wa bei za hisa 30 kubwa zinazofanyiwa biashara katika Soko la Hisa la NewYork NYSE na NASDAQ.
- DAX ni fahirisi ya ‘blue-chip’ ya Kijerumani, inayojumuisha kampuni 30 za Kijerumani kulingana na mtaji wao wa soko.
- UK 100 hujulikana pia kama FTSE 100, au ‘Footsie’. Fahirisi ya bei za hisa za kampuni kubwa 100 zilizoorodheshwa katika Soko la Hisa la London (LSE) kulingana na mtaji wa soko.
- Nikkei 225 ni fahirisi inayoongoza katika soko la hisa la Japan jijini Tokyo.
- Hang Seng Index ni fahirisi huru ya soko la hisa jijini Hong Kong, iliyopangwa kulingana na ukubwa wa mtaji wa soko.
