Sarafu za Kidigitali ni rasilimali za kidigitali zinazoendeshwa na watu wengi, kwa msingi wa teknolojia ya blockchain, na zinazolindwa kupitia kriptografia. Tofauti na sarafu za kawaida ambazo pesa huingizwa kwenye mzunguko wa fedha na ‘Quantitative Easing’ (QE), sarafu za kidigitali hutengenezwa katika blockchains asilia tofauti, huku bei zake zikiathiriwa tu kwa ugavi na mahitaji.

Kuna zaidi ya masoko 25 yanayotoa huduma ya ununuzi, uuzaji na ubadilishaji wa sarafu tofauti za kidigitali, chati zikionyesha zaidi ya sarafu 200. Taarifa ya bei katika sarafu hizi kidesturi huwakilishwa na Dola ya Marekani.

Taarifa ambazo wafanyabiashara na wawekezaji wanaweza kukusanya kutoka kwenye chati hizi za bei, zinaweza kutumika katika chambuzi msingi na za kiufundi, pamoja na katika kufanya uchunguzi zaidi wa miondoko ya bei za sarafu.

Taarifa inayoonyeshwa huhusiana na mtaji wa soko, utohozi kamili wa mtaji wa soko, bei ya hivi karibuni zaidi ya sarafu katika ufungaji soko wa kipindi cha mwisho, ugavi wa sarafu uliopo, jumla ya ugavi ama kiwango cha juu cha ugavi, jumla ya ujazo uliofanyiwa biashara, na % ya mabadiliko ya bei baina ya bei ya ufunguaji na bei ya ufungizi katika kipindi cha mwisho cha biashara.

Wafanyabiashara wanaweza kutumia chati hii ya bei kuchambua ubadilifu na kutathmini utendaji wa sarafu ya kidigitali kwa kuchagua vipindi tofauti vya mida. Viashiria vingi vya kiufundi vinaweza kutumika kutambua mwelekeo wa mwenendo na hali zilizopo katika soko.